Mwokozi Wangu Yesu
Mwokozi Wangu Yesu Lyrics
Mwokozi wangu Yesu hakika unanipenda
Umenilisha mwili na damu umeninywesha
(Yesu) Yesu asante sana sana nakushukuru
Yesu asante sana sana nakushukuru
- Bwana wangu Yesu hakika ninakupenda sana
Moyo wangu mimi ninakutolea wewe Yesu
Umenikaribisha mimi katika karamu hiyo
Karamu ya chakula kilichoshuka toka mbinguni
- Mwili wake Yesu chakula cha roho zetu sisi
Damu yake Yesu kinywaji cha roho zetu sisi
Wana heri wale wote wanaokula mwili wake
Na kuinywa damu yake maana wataishi na Yesu
- Umenipa mwili na damu yako umeninywesha
Umenishibisha na pia umeniburudisha
Umeniimarisha najua sitapata njaa
Hata kiu sitapata nikiwa na wewe Yesu wangu
- Mwamba wangu mimi ni wewe Yesu Mwokozi wangu
Nguvu zangu mimi ni wewe Yesu Mwokozi wangu
Nakutegemea Yesu najua sitaaibika
Na matumaini yangu nifike mbinguni kwako wewe