Mwokozi Wangu Yesu

Mwokozi Wangu Yesu
ChoirSt. Joseph Migori
CategoryEkaristia (Eucharist)
ComposerAlfred Ossonga

Mwokozi Wangu Yesu Lyrics

Mwokozi wangu Yesu hakika unanipenda
Umenilisha mwili na damu umeninywesha
(Yesu) Yesu asante sana sana nakushukuru
Yesu asante sana sana nakushukuru

 1. Bwana wangu Yesu hakika ninakupenda sana
  Moyo wangu mimi ninakutolea wewe Yesu
  Umenikaribisha mimi katika karamu hiyo
  Karamu ya chakula kilichoshuka toka mbinguni
 2. Mwili wake Yesu chakula cha roho zetu sisi
  Damu yake Yesu kinywaji cha roho zetu sisi
  Wana heri wale wote wanaokula mwili wake
  Na kuinywa damu yake maana wataishi na Yesu
 3. Umenipa mwili na damu yako umeninywesha
  Umenishibisha na pia umeniburudisha
  Umeniimarisha najua sitapata njaa
  Hata kiu sitapata nikiwa na wewe Yesu wangu
 4. Mwamba wangu mimi ni wewe Yesu Mwokozi wangu
  Nguvu zangu mimi ni wewe Yesu Mwokozi wangu
  Nakutegemea Yesu najua sitaaibika
  Na matumaini yangu nifike mbinguni kwako wewe