Na Ahimidiwe Bwana
Na Ahimidiwe Bwana | |
---|---|
Alt Title | Enyi Watumishi wa Bwana |
Performed by | Kwaya Kuu ya St. Cecilia Arusha |
Album | Nikiziangalia Mbingu (vol 18) |
Category | Entrance / Mwanzo |
Composer | P. F. Mwarabu |
Views | 6,715 |
Na Ahimidiwe Bwana Lyrics
Enyi watumishi wa Bwana sifuni
Lisifuni lisifuni Jina la Bwana
Na ahimidiwe Bwana Mungu
Bwana Mungu kutoka Sayuni
Akaaye Yerusalemu aleluya- Ninyi msimamao nyumbani mwa Bwana
Nyuani mwa nyumba ya Mungu wenu
Msifuni Bwana kwa kuwa yu mwema
Liimbieni jina lake kwa maana lapendeza - Kwa sababu Bwana amejichagulia Yakobo
Na Israeli wawe watu wake hasa
Maana najua mimi ya kuwa Bwana ni mkuu
Na Mungu wetu yu juu ya miungu yote - Enyi mlango wa Israeli mhimidini
Enyi mlango wa Haruni mhimidini
Enyi mlango wa Lawi himidini Bwana
Enyi mnaomcha Bwana mhimidini Bwana