Nainua Moyo Wangu
Nainua Moyo Wangu | |
---|---|
Performed by | St. Joseph Cathedral Dar-es-Salaam |
Category | General |
Composer | (traditional) |
Views | 29,520 |
Nainua Moyo Wangu Lyrics
- Nainua moyo wangu kwako wewe ee Baba,
Unikinge na uovu, tumaini wewe tu - Nijulishe njia zako nifundishe ukweli
Hekimayo niongoze, tumaini wewe tu - Ee Baba ukumbuke wema wako milele,
Nifutie dhambi zangu, tumaini wewe tu - Nitazame kwa huruma ewe Mungu amini,
Nitubishe mwenye dhambi, tumaini wewe tu - Shida zangu angalia, niokoe dhikini
Nisamehe dhambi zangu, tumaini wewe tu - Njia zako zote Bwana nifadhili na kweli
Niongoze mtoto wako, tumaini wewe tu