Nasikia Sauti Nzuri

Nasikia Sauti Nzuri
Performed byBlessed Virgin Sisters (Tabaka Kisii)
AlbumNaisikia Sauti Nzuri
CategoryInjili na Miito (Gospel)
ComposerAlfred Ossonga
Views40,504

Nasikia Sauti Nzuri Lyrics

  1. Nasikia sauti nzuri, kama ya malaika,
    Ni sauti toka mbinguni, sauti ya Mungu,
    Aniita mimi niende nikamtumikie,
    Anitume shambani mwake, nikavune yote.

    { Umeniita, nimeitika wito, nakuja kwako leo,
    Najongea mbele zako, Bwana nipokee mimi,
    Niko tayari nimeyaacha yote najikabidhi kwako
    Unitume popote nami nitakwenda haraka } *2

  2. Ninaenda mimi naenda, ninaenda mwenyewe
    Ninaenda mbele za Bwana, sitarudi nyuma
    Ndugu zangu na marafiki mniache niende,
    Nikafanye kazi ya Bwana, nitakapotumwa.
  3. Nilitazama moyo wako, moyo wako mwanangu
    Hata kabla hujazaliwa nilikutambua,
    Nilikuteua mapema, kati ya ndugu zako,
    Uwe kuhani wangu mimi, kuhani mkuu.
  4. Shamba lake Bwana ni kubwa, na mavuno ni mengi,
    Wavunaji ndio wachache, nitakwenda mimi.
    Twakuomba sana ee Bwana, tupeleke shambani
    Tukavune mavuno yote, yaliyo tayari.
  5. Uwe nami siku kwa siku, Bwana usiniache
    Unikinge na majaribu, nilinde daima,
    Nipeleke habari njema, ulimwenguni mwote,
    Watu wote wakutambue, wakugeukie.