Nakaza Mwendo
Nakaza Mwendo | |
---|---|
Alt Title | Sio Kwamba |
Performed by | Kwaya Kuu ya St. Cecilia Arusha |
Album | Nakaza Mwendo (Vol 19-20) |
Category | Faith |
Composer | G. C. Mkude |
Views | 22,401 |
Nakaza Mwendo Lyrics
Siyo kwamba nimekwishafika
Au nimekwisha kamilika la! la!
{ Bali ninakaza mwendo ili nipate kulishika
Lile ambalo limeshikwa naye Kristu } *2- Ninaendelea mbele mimi, katika utumishi wangu
Nijalie nguvu Bwana wangu, niyashinde haya ya dunia - Nishike mkono Bwana wangu, shetani asinisumbue
Niongoze vyema Bwana wangu, niyashike majukumu yangu - Nitashinda mimi nitashinda, nitashinda kwa nguvu zako
Ninatarajia ushujaa, endapo wewe utaamua - Nitavikwa mimi nitavikwa, nitavikwa taji ya hadhi
Sio kwa nguvu zangu mwenyewe bali kwa nguvu za Mungu Baba - Aleluya nitaimba mimi, nitakapomaliza safari
Hayo ni matarajio yangu, mwisho wa hii safari yangu