Nakula Mwili wa Yesu
Nakula Mwili wa Yesu | |
---|---|
Alt Title | Naimba Wimbo wa Yesu |
Performed by | Our Lady(Star of the Sea) Kenya Navy |
Category | Ekaristia (Eucharist) |
Composer | Alfred Ossonga |
Views | 15,326 |
Nakula Mwili wa Yesu Lyrics
- Nakula mwili wa Yesu, nakunywa damu ya Yesu
Naburudika daima, narukaruka na Yesu
Naimba wimbo wa Yesu, nachezacheza na Yesu
Natembea naye Yesu, naenda kwetu Mbinguni{ Mimi nashangalia, (mimi) mimi naburudika
Yesu ameniponya, kweli nina uzima } *2 - Mwalimu wangu ni Yesu, tabibu wangu ni Yesu
Mlinzi wangu ni Yesu, mimi nina usalama
Uhai wangu ni Yesu, mapito yangu ni Yesu,
Naenda na Bwana Yesu, naelekea Mbinguni - Rafiki wangu ni Yesu, jabali wangu ni Yesu
Mshindi wangu ni Yesu, mimi nitashinda vita.
Mpaji wangu ni Yesu , mlishi wangu ni Yesu
Mjali wangu ni Yesu, sina budi kumsifu - Kaeni ndani ya Yesu, kaeni pamoja naye
Na Yesu akae kwenu, mtashinda majaribu
Shikeni maneno yake, jifunzeni kwake Yesu
Yesu atawachukua, awapeleke Mbinguni - Maisha ya duniani, pasipo Yesu ni bure
Uzima wa ulimwengu, bila Yesu ni hapana
Kuleni mwili wa Yesu, kunyweni damu ya Yesu
Onjeni damu ya Mbingu, mtaishi siku zote