Nakula Mwili wa Yesu

Nakula Mwili wa Yesu
Alt TitleNaimba Wimbo wa Yesu
ChoirOur Lady(Star of the Sea) Kenya Navy
CategoryEkaristia (Eucharist)
ComposerAlfred Ossonga

Nakula Mwili wa Yesu Lyrics

 1. Nakula mwili wa Yesu, nakunywa damu ya Yesu
  Naburudika daima, narukaruka na Yesu
  Naimba wimbo wa Yesu, nachezacheza na Yesu
  Natembea naye Yesu, naenda kwetu Mbinguni

  { Mimi nashangalia, (mimi) mimi naburudika
  Yesu ameniponya, kweli nina uzima } *2

 2. Mwalimu wangu ni Yesu, tabibu wangu ni Yesu
  Mlinzi wangu ni Yesu, mimi nina usalama
  Uhai wangu ni Yesu, mapito yangu ni Yesu,
  Naenda na Bwana Yesu, naelekea Mbinguni
 3. Rafiki wangu ni Yesu, jabali wangu ni Yesu
  Mshindi wangu ni Yesu, mimi nitashinda vita.
  Mpaji wangu ni Yesu , mlishi wangu ni Yesu
  Mjali wangu ni Yesu, sina budi kumsifu
 4. Kaeni ndani ya Yesu, kaeni pamoja naye
  Na Yesu akae kwenu, mtashinda majaribu
  Shikeni maneno yake, jifunzeni kwake Yesu
  Yesu atawachukua, awapeleke Mbinguni
 5. Maisha ya duniani, pasipo Yesu ni bure
  Uzima wa ulimwengu, bila Yesu ni hapana
  Kuleni mwili wa Yesu, kunyweni damu ya Yesu
  Onjeni damu ya Mbingu, mtaishi siku zote