Nampenda Bwana Mungu
| Nampenda Bwana Mungu | |
|---|---|
| Performed by | St. Paul Students' Choir (University of Nairobi) |
| Album | Tazameni Miujiza (Vol 2) |
| Category | Zaburi |
| Composer | J. C. Shomaly |
| Views | 4,927 |
Nampenda Bwana Mungu Lyrics
{Nampenda Bwana Mungu wangu kwa maana yeye amenisikia
Ameyasikia maombi yangu sala zangu pia nazo dua zangu } *2
{ Nilipokuwa tabuni Bwana alinishika mkono (wangu)
Kifo kiliponisonga akaniokoa } *2- Nilipata huzuni na masumbuko mengi ya duniani
Nikalia Bwana akakisikia kilio kilio changu - Adui zangu waliponikaribia waliniogopa,
Kwa sababu Bwana alikuwa karibu karibu yangu mimi - Sasa nafurahia kwa sababu Bwana amenipenda
Naimba na nyimbo nzuri nikili-sifu jina la Bwana