Login | Register

Sauti za Kuimba

Nampenda Bwana Mungu Lyrics

NAMPENDA BWANA MUNGU

@ J. C. Shomaly

{Nampenda Bwana Mungu wangu kwa maana yeye amenisikia
Ameyasikia maombi yangu sala zangu pia nazo dua zangu } *2
{ Nilipokuwa tabuni Bwana alinishika mkono (wangu)
Kifo kiliponisonga akaniokoa } *2

  1. Nilipata huzuni na masumbuko mengi ya duniani
    Nikalia Bwana akakisikia kilio kilio changu
  2. Adui zangu waliponikaribia waliniogopa,
    Kwa sababu Bwana alikuwa karibu karibu yangu mimi
  3. Sasa nafurahia kwa sababu Bwana amenipenda
    Naimba na nyimbo nzuri nikili-sifu jina la Bwana
Nampenda Bwana Mungu
COMPOSERJ. C. Shomaly
CHOIRSt. Paul Students' Choir (University of Nairobi)
ALBUMTazameni Miujiza (Vol 2)
CATEGORYZaburi
REFPs. 116
MUSIC KEYD Major
TIME SIGNATURE3
8




  • Comments