Nani Kama Mama
Nani Kama Mama | |
---|---|
Performed by | Our Lady(Star of the Sea) Kenya Navy |
Album | Tumeandamana |
Category | Bikira Maria |
Composer | Alfred Ossonga |
Views | 7,117 |
Nani Kama Mama Lyrics
- Kwa ujasiri kwa sauti kubwa,
nazitangaza sifa za mama [Maria]
Nawauliza wakubwa wadogo,
Ni nani kama mama [Maria]Alimzaaa Mungu mwenyewe [kweli]
amewakomboa wana wa Eva [wote]
Mama Maria anatuombea kwenye safari
tufike salama [Mama Maria]
Atungojea kule kwa mwanaye
atupokee tuishi salama *2 - Kwa sifo tele kwa shangwe nderemo,
Tujitokeze mbele za mama [Maria]
Tucheze ngoma tupige makofi,
vigelegele heko kwa mama [Maria] - Salamu Mama umebarikiwa,
Na baraka kuliko wote [Maria]
Mzao wako amebarikiwa,
Yesu mwanao ni Mungu kweli [Maria] - Tukimbilie ulinzi wa mama,
Tufunuliwe siri za Mbingu[Maria]
Tupate shibe tupate neema,
Tuwe na heri hata milele [Maria]