Nani Kama Mama Lyrics

NANI KAMA MAMA

@ Alfred Ossonga

 1. Kwa ujasiri kwa sauti kubwa,
  nazitangaza sifa za mama [Maria]
  Nawauliza wakubwa wadogo,
  Ni nani kama mama [Maria]

  Alimzaaa Mungu mwenyewe [kweli]
  amewakomboa wana wa Eva [wote]
  Mama Maria anatuombea kwenye safari
  tufike salama [Mama Maria]
  Atungojea kule kwa mwanaye
  atupokee tuishi salama *2

 2. Kwa sifo tele kwa shangwe nderemo,
  Tujitokeze mbele za mama [Maria]
  Tucheze ngoma tupige makofi,
  vigelegele heko kwa mama [Maria]
 3. Salamu Mama umebarikiwa,
  Na baraka kuliko wote [Maria]
  Mzao wako amebarikiwa,
  Yesu mwanao ni Mungu kweli [Maria]
 4. Tukimbilie ulinzi wa mama,
  Tufunuliwe siri za Mbingu[Maria]
  Tupate shibe tupate neema,
  Tuwe na heri hata milele [Maria]
Nani Kama Mama
COMPOSERAlfred Ossonga
CHOIROur Lady(Star of the Sea) Kenya Navy
ALBUMTumeandamana
CATEGORYBikira Maria
 • Comments