Nani ni Nani

Nani ni Nani
Alt TitleNi Nani Kama Mungu
Performed byKwaya Kuu ya St. Cecilia Arusha
AlbumMSHIPI (VOL. 22)
CategoryEntrance / Mwanzo
ComposerR. Masanja
Views23,087

Nani ni Nani Lyrics

  1. Nani ni nani, ni nani ni nani,
    Ni nani ni nani, nani kama Mungu
    Mwenye uwezo, na mwenye ukuu
    Ni nani ni nani nani kama Mungu

  2. Ameniumba, jinsi nilivyo, nipendezavyo ni nani kama Mungu
    Niseme nini, niimbe nini, nilie vipi, ni nani kama Mungu
  3. Tazama jua, mwezi na nyota, mbingu na nchi . . .
    Nao usiku, jua li wapi, ni maajabu ni nani kama Mungu
  4. Ananilinda, mchana kutwa, pia usiku, ni nani kama Mungu
    Nikitembea, nikisimama, ananilinda , ni nani kama Mungu
  5. Tazama ndege wa msituni wanavyoishi , ni nani kama Mungu Hawana shamba wala vilenge anawalisha , ni nani kama Mungu
  6. Na maarifa, tuliyonayo, yeye katupa, ni nani kama Mungu
    Njooni pamoja, tumuimbie, na tumsifu, ni nani kama Mungu