Nasadiki (Misa Imani)
| Nasadiki (Misa Imani) |
|---|
| Performed by | - |
| Category | TBA |
| Views | 3,555 |
Nasadiki (Misa Imani) Lyrics
Ninasadiki ninasadiki - sadiki
Nasadiki kwa Mungu Baba, mwumba wa vyote
Nasadiki kwa Yesu Kristu, mwana wa pekee
- Bikira Maria kawa mamaye
Kwa uwezo wa Roho, Mungu mtakatifu
- Kisha akasulubiwa kwa ajili yetu
Kwa amri ya Ponsyo Pilato,
- Siku ya tatu kafufuka kutoka kwa wafu
Ameketi kuume kwake Mungu Baba
- Siku ya mwisho atarudi kutuhukumu
Nasadiki kwa Mungu Roho Mtakatifu
- Kanisa pia takatifu Katoliki
Ushirika wa watakatifu nasadiki
- Ondoleo la dhambi kwa ubatizo
fufuko wa miili, uzima wa milele