Nasadiki (Misa Voi)
Nasadiki (Misa Voi) |
---|
Performed by | - |
Category | TBA |
Views | 3,369 |
Nasadiki (Misa Voi) Lyrics
- Nasadiki kwa Mungu Baba mwenyezi
Mungu mmoja muumba mbingu na dunia
Nasadiki na kwa Bwana Yesu Kristu
Aliye mwana wa pekee wa Mungu
Ninasadiki, ninasadiki
Kazaliwa kwa Baba tangu milele
Mwanga kwa mwanga kweli Mungu kwa Mungu
Mwenye U-Mungu Mmoja sawa na baba
Kashuka toka mbinguni kutokoa
- Akapokea mwili sawa na sisi
Kwa uwezo wake roho mtakatifu
Akazaliwa naye bikira maria
Akateswa pia akasulubiwa
- Yote hayo ni kwa ajili yet utu
Akazikwa halafu akafufuka
Akapaa mbinguni kwa Baba yake
Atarudi tena kwa utukufu mkuu
- Kuwahukumu wazima pia na wafu
Ufalme wake hautakuwa na mwisho
Nasadiki kwa roho mtakatifu
Yeye ni Bwana pia mleta uzima
- Atokaye kwa Baba vile kwa mwana
Aliyenena kwa vinywa vya manabii
Nasadiki kwa kanisa lililo moja
Takatifu Katoliki na la mitume
- Naungama pia ubatizo mmoja
Kwa ajili ya maondoleo ya dhambi
Nangojea na ufufuko wa wafu
Na uzima wa milele ijayo, amina