Nasadiki kwa Mungu (Baba Mwenyezi)
Nasadiki kwa Mungu (Baba Mwenyezi) |
---|
Performed by | - |
Category | TBA |
Views | 30,171 |
Nasadiki kwa Mungu (Baba Mwenyezi) Lyrics
Nasadiki kwa Mungu Baba Mwenyezi (Muumba)
Mbingu na nchi na kwa Yesu Kristu
- Mwana wa pekee wa Mungu
Mwenye kuzaliwa kwa Baba
Akapata mwili kwa Roho
Kazaliwa naye Bikira
- Kisha yeye kasulubiwa
Kwa amri ya Ponsio Pilato
Kwa ajili yetu kateswa
Akafa na akazikwa
- Kafufuka katika wafu
Kapaa juu Mbinguni
Ameketi kuume kwake
Mungu Baba yetu mwenyezi
- Ndipo atakapotokea
Kuhukumu wazima na wafu
Kwake Roho Mtakatifu
Kwa kanisa la Katoliki
- Ushirika wa watakatifu
Ondoleo la dhambi zetu
Nangojea ufufuko wa miili
Na uzima wa milele