Nasadiki Kwa Mungu (Mbingu na Dunia)
Nasadiki Kwa Mungu (Mbingu na Dunia) |
---|
Performed by | - |
Category | TBA |
Views | 5,334 |
Nasadiki Kwa Mungu (Mbingu na Dunia) Lyrics
- Nasadiki kwa Mungu mmoja, Mwumba Mbingu na dunia
Na kwa Yesu Kristu mwanaye, Wa pekee Bwana wetu
Nasadiki ninasadiki kweli ninasadiki
Nasadiki kwa Mungu Mmoja
- Akapata mwili kwa tendo, Lake Roho Mtakatifu
Kazaliwa naye Bikira, Akateswa kwa Ponsio Pilato
- Akasulubiwa akafa, Akazikwa kaburini
Na kuzimu akashukia, Kafufuka siku ya tatu
- Akapaa juu Mbinguni, Ameketi kuume kwake
Mungu Baba yetu Mwenyezi, Muumba Mbingu na dunia
- Ndipo atakapotokea, Kuhukumu wazima na wafu
Na uzima wake milele, Utadumu bila mwisho
- Nasadiki kanisa ni moja, Ni kanisa takatifu
Ni kanisa la Katoliki, Ni kanisa la mitume
- Ushirika wa watakatifu, Ondoleo la dhambi zetu
Nangojea ufufuko wa mwili, Na uzima wa milele