Nasimulia Sifa
| Nasimulia Sifa | |
|---|---|
| Performed by | St. Paul Students' Choir (University of Nairobi) |
| Album | Mbinguni Kutakuwa Raha (Vol 4) |
| Category | Thanksgiving / Shukrani |
| Composer | J. C. Shomaly |
| Views | 4,872 |
Nasimulia Sifa Lyrics
{ Nasimulia sifa za Bwana Mungu, tena na maajabu
kwa viumbe wa duniani Mungu ni mtawala } *2
Nashangaa lo! nashangaa lo! *2
{ Viwete wamepona, viziwi wamesikia,
Bubu wamesemasema Mungu ni mtawala,
kazi yake hutenda kwa haki } *2- Kakusanya maji chungu chungu, maji ya bahari,
Karatibisha udongo wenye rutuba - Mwanga pia giza, kazitoa kwa ratiba yake,
Mchana wa jua, usiku wa mbalamwezi - Miti ya matunda, mingine isiyo na matunda,
Mingine mirefu, mingine mifupi sana - Enyi watu wote mwimbieni mwimbieni Mungu
Lisifuni jina lake Mungu wa miungu.