Login | Register

Sauti za Kuimba

Nasimulia Sifa Lyrics

NASIMULIA SIFA

@ J. C. Shomaly

{ Nasimulia sifa za Bwana Mungu, tena na maajabu
kwa viumbe wa duniani Mungu ni mtawala } *2

Nashangaa lo! nashangaa lo! *2
{ Viwete wamepona, viziwi wamesikia,
Bubu wamesemasema Mungu ni mtawala,
kazi yake hutenda kwa haki } *2

 1. Kakusanya maji chungu chungu, maji ya bahari,
  Karatibisha udongo wenye rutuba
 2. Mwanga pia giza, kazitoa kwa ratiba yake,
  Mchana wa jua, usiku wa mbalamwezi
 3. Miti ya matunda, mingine isiyo na matunda,
  Mingine mirefu, mingine mifupi sana
 4. Enyi watu wote mwimbieni mwimbieni Mungu
  Lisifuni jina lake Mungu wa miungu.
Nasimulia Sifa
COMPOSERJ. C. Shomaly
CHOIRSt. Paul Students' Choir (University of Nairobi)
ALBUMMbinguni Kutakuwa Raha (Vol 4)
CATEGORYThanksgiving / Shukrani
MUSIC KEYD Major
TIME SIGNATURE3
8
 • Comments