Natamani Uwe Wangu
Natamani Uwe Wangu Lyrics
- Nimekupenda nimevutiwa na wewe sikia-
Ninatamani niwe wako uwe wangu siku zote
Ndiwe chaguo la moyo wangu kwenye hii dunia-
Ninatamani niwe wako uwe wangu siku zote
Nitakusifu bila aibu hadharani (wewe)
Nyimbo za shangwe hazitakauka kinywani
(mwangu) Ingia mwangu,
Yesu wangu kaa nami siku zote
- Nimewaona rafiki wengi wanaonivizia-
Lakini wewe ndiye rafiki wa kweli na huria-
- Ulinipenda hata kabla mimi sijakusikia-
Msalabani bila hatia Yesu ukanifia-
- Katika raha usikawie njoo kufurahia--
Na kwenye shida sitachelewa nitakukimbilia--
- Nitakusifu milele yote nitakuhimidia--
Nitaziimba fadhili zako nitazisimulia--