Navumilia Tu

Navumilia Tu
Performed byBlessed Joseph Allamano Mshindo Iringa
AlbumWatu Wamekengeuka
CategoryKwaresma na Toba (Lent & Repentance)
ComposerF. F. Ngwila
Views23,847

Navumilia Tu Lyrics

  1. [s/a] Ninatazama juu angani nikiomba msaada
    Mateso yananizidi, hakuna anayekuja
    Nafungua mikono yangu naleta sala yangu
    Ee Bwana nisaidie, Mungu unihurumie
    Navumilia tu mimi ninavumilia tu
    (Bwana nateseka)

    /s/
    Navumilia tu, mimi ninavumilia tu,
    Navumilia tu, kwani haya yote yana mwisho
    Navumilia tu, mimi ninavumilia tu,
    Navumilia tu, kwani ipo siku yatakwisha

    /a2/
    Navumilia tu, ninavumilia tu mimi
    Navumilia tu, kwani haya yote yana mwisho
    Navumilia tu, ninavumilia tu mimi
    Navumilia tu, kwani ipo siku yatakwisha

    / t2 / a1 /
    Bwana nateseka, unihurumie kwa uwezo wako
    Naamini Bwana
    Nipo kwenye shida, Bwana niokoe sikati tamaa,
    Naamini Bwana, ipo siku yatakwisha

    /t/
    Navumilia tu mimi, ninavumilia tu
    Navumilia tu, kwani haya yote yana mwisho
    Navumilia tu mimi, ninavumilia tu
    Navumilia tu, kwani ipo siku yatakwisha

    /b/
    Navumilia tu mimi, navumilia tu mimi
    Navumilia tu, haya yote yana mwisho
    Navumilia tu mimi, navumilia tu mimi
    Navumilia tu, ipo siku yatakwisha

  2. Nalia kwa uchungu, machozi yananitiririka,
    Mateso ya dunia hii, naona yamekidhiri,
    Huyu mwovu shetani hakika ananisonga sana
    Ninakuomba ee Bwana unisaidie hima
    Navumilia tu mimi ninavumilia tu
    (Bwana nateseka)
  3. Vitisho vya dunia, magonjwa dharau masengenyo
    Na kunyanyasa wadogo, haya yote yatapita
    Nangojea kwa hamu, Bwana utakapokuja tena
    Nije niungane nawe, kwenye raha ya milele
    Navumilia tu mimi ninavumilia tu
    (Bwana nateseka)
  4. Ewe mama Maria, naomba uniombee mama
    Kwa Yesu mwanao mpenzi, ili aje aniokoe
    Roho mtakatifu Mungu anipe ujasiri,
    Hekima na pia nguvu, elimu pia uchaji
    Navumilia tu mimi ninavumilia tu
    (Bwana nateseka)
*Kwa wote walio katika taabu, uchungu na mateso ya aina yoyote; hasa WAGONJWA - ''Usikate tamaa, Mungu atasikia sala yako na atakufanyia miujiza. Ipo siku yatakwisha.''