Nawapa Amri
Nawapa Amri |
---|
Performed by | - |
Category | Love |
Views | 15,773 |
Nawapa Amri Lyrics
Nawapa amri - amri pendaneni (asema Bwana )
{ Kama vile mimi nilivyowapenda nyinyi
(Nanyi) Nanyi pia mpendaneni } *2
- Wapenzi na tupendane, neno latoka kwa Mungu
Na pia apendaye amezaliwa na Mungu,
(Naye) Naye anamjua Mungu, tupendane
- Yule asiye na pendo, hakumjua Mungu wetu
Kwa maana Mungu ni mwenye upendo kamili
(Naye) Naye ametuamuru, tupendane
- Mungu apenda dunia kwa mapendo yake kwetu
Akamtuma mwanaye mwana wake wa pekee
(Hapa) Hapa kwetu duniani, tupendane
- Kila amkiriye Yesu, kuwa ni mwana wa Mungu
Ndipo Mungu anakaa, ndani yake mtu yule
(Naye) Naye ndani yake Mungu, tupendane