Ndimi Mtumishi wako
| Ndimi Mtumishi wako | |
|---|---|
| Performed by | - | 
| Category | Thanksgiving / Shukrani | 
| Views | 16,510 | 
Ndimi Mtumishi wako Lyrics
- Ndimi mtumishi wako,
 Nitafurahi kwako Bwana (mimi) *2
- Nitajongea altare ya Mungu,
 Mungu wa raha ya roho yangu
- Machoni pangu meza imepambwa,
 wanatazama adui zangu
- Malishoni mwa majani mabichi,
 ananitunza nikiwa naye
- Sifa ziende kwa Baba na Mwana,
 na kwake Roho milele yote
 
  
         
                            