Ndiwe Sitara Yangu

Ndiwe Sitara Yangu
Performed bySt. Augustine JKUAT
CategoryZaburi
Views4,516

Ndiwe Sitara Yangu Lyrics

  1. Ndiwe sitara yangu utanihifadhi na mateso
    Unanizungushia nyimbo za wokovu

  2. Heri aliyesamehewa dhambi na kusitiriwa makosa yake
    Heri Bwana asiyemhesabia upotovu
    Ambaye moyoni mwake hamna hila
  3. Walikujulisha dhambi yangu
    wala sikuuficha upotovu wangu
    Nalisema nitakiri maasi yangu kwa Bwana
    Nawe ukanisamehe upotovu wa dhambi yangu
  4. Mfurahieni Bwana, shangilieni enyi wenye haki
    Pigeni vigelegele vya furaha
    Nyinyi nyote mlio wanyofu wa moyo