Ndugu Kaza Mwendo
Ndugu Kaza Mwendo | |
---|---|
Performed by | Kwaya Kuu ya St. Cecilia Arusha |
Album | MSHIPI (VOL. 22) |
Category | Tafakari |
Composer | F. Mtegeta |
Views | 11,087 |
Ndugu Kaza Mwendo Lyrics
Ndugu yangu kaza mwendo Safari bado ni ndefu
{Ina mabonde mengi pia na milima (mingi)
Ina wanyama wengi tena wa kutisha (sana)
Usilege'legee kaza mwendo tutafika.}*2- Usali na kuomba ufike salama
Kwa maana safari yetu ina vikwazo vingi
Kuna mbwa mwitu wanaonyemelea roho za watu *2 - Tunza imani yako usiyumbeyumbe
Tena usikate tamaa kumuabudu Muumba wako
Parapanda itakapolia ikukute u tayari *2 - Ole wanafiki na wagombanishi
Kwa sababu hukumu yaja kwa wasiopenda amani
Watakuja lia na kusaka meno siku ya hukumu *2