Ngoja Nicheze
   
    
     
         
          
            Ngoja Nicheze Lyrics
 
             
            
- Tazama mimi ninavyopumua,
 Tazama mimi nilivyo na nguvu
 Tazama mimi ninavyopumua,
 Tazama mimi nilivyo na nguvu
 Hizo zote - ni neema bure toka kwa Mungu
 Na mimi leo - ngoja nicheze muone,
 Nitamsifu ngoja nicheze muone,
 Bila kuchoka - ngoja nicheze muone aee
- Tazama mimi nakula na kushiba,
 Tazama mimi nalala nasinzia
 Tazama naamka mimi mwenyewe e,
 Tazama tazama ah tazama aa aha
- Tazama mimi naweza kuongea,
 Tazama mimi naimba bila shida
 Tazama naweza kucheza mwenyewe e
 Tazama tazama ah tazama aa aha
- Nikiugua ona napewa pole,
 ninapofiwa ndugu mwanifariji
 Tazama niwapo na shida wanajaa a
 Tazama tazama ah tazama aa aha
- Nikikosea huwa nasamehewa,
 Nikiudhiwa ndugu mwanitetea
 Tazama dhuluma haitaniua a
 Tazama tazama ah tazama aa aha
- Nikifurahi ndugu washerehekea,
 Nikiudhiwa ndugu wasononeka
 Tazama ninaishi kati ya watu u
 Tazama tazama ah tazama aa aha
- Na yote haya najaliwa na Mungu,
 Amenipenda upeo wa upendo
 Tazama na mimi nitamtukuza a
 Tazama tazama ah tazama aa aha