Ngong Ngong

Ngong Ngong
Performed bySt. Joseph Migori
AlbumNitachezacheza
CategoryEntrance / Mwanzo
ComposerAlfred Ossonga
Views10,814

Ngong Ngong Lyrics

  1. [s:] Ngong ngong ninagonga ee Bwana nisikie
    [w:] Nimo malangoni ninakuita
    [s:] Ngong ngong ninagonga mlango wako Bwana
    [w:] Bwana nipokee nikaribishe
    [s:] Nasikia kwa Bwana kuna chakula
    [w:] Nimekuja Bwana unishibishe
    [s:] Nasikia ya kwamba kuna kinywaji
    [w:] Nimekuja leo niburudike
    [s:] Bwana unipokee nisikilize
    [w:] Unipe neema unibariki

  2. Nyumba yake Bwana ni nyumba ya sala, endeni
    kwa heshima, tukaijongee meza ya mapendo, kwa furaha
  3. Nyumbani mwa Bwana mna neema nyingi nendeni
    mkapewe, tuugonge mlango wake pamoja, tuingie
  4. Bwana nimekuja leo na mapema, Mbele ya nyumba
    yako, unikaribishe hekaluni mwako, nakuomba
  5. Sala zangu na dua zangu natoa Bwana zikufikilie
    Unifungulie masikio yako siku zote