Ni Nani Kama Mungu

Ni Nani Kama Mungu
Performed bySt. Cecilia Zimmerman
CategoryGeneral
Views6,208

Ni Nani Kama Mungu Lyrics

 1. Ni nani awezaye kufananishwa na Mungu
  Ni kitu gani kiwezacho kufananishwa na Muumba*2
  Wiki nzima amenipa nguvu amenipa na uhai
  Nimefanya kazi zangu zote kwa ratiba zangu zote
  Na sasa niko hapa mbele kuutangaza wema wake
  Waumini simameni-pigeni vigelegele
  Na tuimbe pamoja tutangaze wema wake

 2. Hebu fikiria ndugu ilivyo maajabu wewe
  Umempa nini Bwana wetu muumba
  Ni wengi waliopenda kuiona siku hii
  Kwa mapenzi yake yeye wote wote hawakuiona
 3. Hebu fikiria pia ilivyo maajabu wewe
  Una maisha bora pia ya kupendeza
  Ni wengi hawana nyumba hawana na makazi
  Viungo vya mwili mikono na hata miguu