Nikiziangalia Mbingu
Nikiziangalia Mbingu | |
---|---|
Performed by | Kwaya Kuu ya St. Cecilia Arusha |
Album | Nikiziangalia Mbingu (vol 18) |
Category | Zaburi |
Composer | G. C. Mkude |
Views | 14,174 |
Nikiziangalia Mbingu Lyrics
{ Nikiziangalia mbingu, ni kazi ya vidole vyako
Mwezi na nyota za Mbinguni, ulizoratibisha wewe } *2- Naye mtu ni kitu gani, hata naye umkumbuke
Naye binadamu ni nani, hata naye umuangalie - Umemfanya punde mdogo ni mdogo kuliko Mungu
Umemvika taji yake, taji ya utukufu na heshima - Umemtawaza juu ya kazi, ni kazi ya mikono yako
Umevitia vitu vyote, chini ya miguu yako ee Bwana - Kondoo nao ng'ombe wote pia wanyama wa kondeni
Ndege wote wa angani na samaki wote wote baharini
~ Key D 2/4 | Kwaya Kuu ya Mt. Cecilia Arusha (KMC)