Nikushukuruje Ee Mungu

Nikushukuruje Ee Mungu
ChoirSt. Benedict Rapogi
AlbumHuyu Ni Yesu (Vol 1)
CategoryThanksgiving / Shukrani

Nikushukuruje Ee Mungu Lyrics

Nikushukuruje ee Mungu - kwa ukarimu wako
Nikushukuruje ee Mungu - kwa mema yako yote
Uliyonijalia, unayonijalia
{Baba asante (ee Baba) asante asante,
(Ee Baba) Asante asante nasema asante *2 }

 1. Tumepokea shibe, kwa mwili na damuyo,
  Kwa mema yako yote twasema asante
 2. Fadhili zako Bwana, huruma yako Bwana
  Watujalia sote twasema asante
 3. Watulinda salama, twendapo na kurudi,
  Mchana na usiku twasema asante
 4. Sote twaimarika, kwa pendo lako kuu
  Ee Baba yetu mwema twasema asante