Nimeahidi Yesu
Nimeahidi Yesu Lyrics
- Nimeahidi Yesu - kukutumikia
Wewe u Bwana wangu - u rafiki pia
Sitaogopa vita - wewe ndiwe mweza
Sitaiacha njia - ukiniongoza
Imbeni aleluya, aleluya, imbeni
Shangwe kwa Bwana Yesu, ndiye mweza wetu
- Dunia i karibu - Bwana siniache
Na mengi majaribu - yako pande zote
Siku zote adui - ni ndani na nje
Bwana Yesu nivute - karibu na wewe
- Nikusikie wewe Bwana - nenda nami Bwana
Kelele za dunia - ndizo nyingi sana
Nena kunihimiza - au kunionya
Nena nikusikie - mwenye kuniponya
- Umewapa ahadi - wakufuatao
Kwenda uliko wewe - wawe huko nao
Nami nimeahidi - kukutumikia
Nipe neema Bwana - ya kukwandamia
- Hatua zako Bwana - na nizikanyage
Wewe u mwenye nguvu - mimi ni mnyonge
Niongoze nivute - nishike daima
Mwishoni niwasili - mbinguni salama