Nimeingia Kwako
| Nimeingia Kwako | |
|---|---|
| Performed by | - | 
| Category | Entrance / Mwanzo | 
| Composer | F. A. Nyundo | 
| Views | 19,821 | 
Nimeingia Kwako Lyrics
- Nimeingia (kwako) hapa mahali patakatifu
 Unipokee (Bwana) unitakase nipate neema
- Nimeingia kwako nimeingia
 Hapa mahali patakatifu
- Ee Bwana mwema wewe mfadhili sana
 Nakuja kwako kukutukuza
- Nakuabudu pia nakusujudu
 Nisaidie mimi ni wako
- Mimi mkristu pokea sala zangu
 Ninakuomba msaada wako
- Nihurumie kwani mimi mnyonge
 Nategemea msaada wako
- Unipokee kwako unipokee
 Unitakase nipate neema
 
  
         
                            