Nimekukimbilia Wewe

Nimekukimbilia Wewe
Performed by-
CategoryGeneral
Views9,298

Nimekukimbilia Wewe Lyrics

  1. Nimekukimbilia wewe wewe Bwana wangu
    Nisiaibike milele nisiaibike milele
    Milele milele nisiaibike nisiaibike milele

  2. Nimekukimbilia wewe nimekukimbilia wewe
    Bwana nisiaibike milele, kwa haki yako uniponye
    Unitegee sikio lako uniokoe hima
  3. Uwe wangu mwamba wa nguvu,
    Nyumba yenye maboma ya kuniokoa,
    Ndiwe genge langu na ngome yangu
    Kwa ajili ya jina lako uniongoze unichunge
  4. Umwangaze mtumishi wako kwa nuru yako
    Uniokoe kwa ajili ya fadhili zako,
    We ni hodari mpige moyo konde
    Ninyi nyote mnaongoja mnaomngoja