Nimempokea Yesu

Nimempokea Yesu
Alt TitleMimi Nimekombolewa
ChoirSt. Joseph Migori
CategoryThanksgiving / Shukrani
ComposerAlfred Ossonga

Nimempokea Yesu Lyrics

(Mimi Nimekombolewa)

 1. Nimempokea Yesu mzima kwenye Ekaristi
  Nguvu zake za mbinguni na baraka amenipa
  Sasa moyo wangu mimi unafurahi
  Roho yangu mimi inashangilia (kweli)

  Mimi nimekombolewa mimi nina uzima wa milele
  Yesu amenikomboa sasa nimekuwa kiumbe kipya
  { Nimempokea Yesu nikajikabidhi kwake
  Aniongoze anifikishe kwake mbinguni } *2

 2. Nimempokea Yesu mzima kwenye maandiko
  Bibilia takatifu kweli nimeisoma
  Mafundisho yake yote yamenigusa
  Nikaamua nijikabidhi kwake (kweli)
 3. Nimempokea Yesu mzima kwenye mahubiri
  Mahubiri yake yamejaa hekima na busara
  Maneno ya kinywa chake ni taa yangu
  Mwanga wa kuniongoza nipitapo (kweli)
 4. Nimempokea Yesu mzima kwenye jumuiya
  Majirani marafiki ndugu zangu na jamaa
  Nyote mnaonijua nawaambia
  Mimi si wenu, mimi ni wake Yesu (kweli)