Mungu Yulee

Mungu Yulee
Alt TitleNimemuona Mungu
Performed bySt. Kizito Makuburi
AlbumMungu Yule
CategoryTafakari
ComposerBernard Mukasa
Views9,816

Mungu Yulee Lyrics

  1. { Nimemuona yule ninayemtafuta na neema zake
    Nimemuona -leo nimemuona Mungu } *2

    Mkononi mwake ana uzima tena ni wa milele
    Mkononi mwake ana uzima ninaoutafuta
    Na uzima huo anatoa bure kwa walio tayari
    Lakini kuna kanuni moja ya kwamba, uwajali watu.

  2. Nimemuona Mungu yu mtupu-u hana nguo
    Anatamani mimi niende nikamvishe
    Nimemuona Mungu ana njaa hana chakula
    Anatamani mimi niende nikamlishe
    Nimemuona Mungu ni mgonjwa-a kitandani
    Anatamani mimi niende kumtazama
  3. Nimemuona Mungu amefungwa-a gerezani
    Anatamani mimi niende kumfariji
    Nimemuona Mungu ni mkimbizi mpakani
    Anatamani mimi niende kumpokea
    Nimemuona Mungu ni yatima hana wazazi
    Anatamani mimi niende nikamtunze
  4. Nimemuona Mungu ni mjane hana matunzo
    Anatamani mimi niende kumhifadhi
    Nimemuona Mungu amefiwa ana majonzi
    Anatamani mimi niende kumfariji
    Nimemuona Mungu ni kilema na hajiwezi
    Anatamani mimi niende kumuinua
  5. Nimemuona Mungu atolewa angali mimba
    Anatamani mimi niende kumtetea
    Nimemuona Mungu anapigwa kwa makombora
    Anatamani mimi niende kusuluhisha
    Nimemuona Mungu ni mtumwa ananyanyaswa
    Anatamani mimi niende kumtetea