Login | Register

Sauti za Kuimba

Mungu Yulee Lyrics

MUNGU YULEE

@ Bernard Mukasa

{ Nimemuona yule ninayemtafuta na neema zake
Nimemuona -leo nimemuona Mungu } *2

Mkononi mwake ana uzima tena ni wa milele
Mkononi mwake ana uzima ninaoutafuta
Na uzima huo anatoa bure kwa walio tayari
Lakini kuna kanuni moja ya kwamba, uwajali watu.

 1. Nimemuona Mungu yu mtupu-u hana nguo
  Anatamani mimi niende nikamvishe
  Nimemuona Mungu ana njaa hana chakula
  Anatamani mimi niende nikamlishe
  Nimemuona Mungu ni mgonjwa-a kitandani
  Anatamani mimi niende kumtazama
 2. Nimemuona Mungu amefungwa-a gerezani
  Anatamani mimi niende kumfariji
  Nimemuona Mungu ni mkimbizi mpakani
  Anatamani mimi niende kumpokea
  Nimemuona Mungu ni yatima hana wazazi
  Anatamani mimi niende nikamtunze
 3. Nimemuona Mungu ni mjane hana matunzo
  Anatamani mimi niende kumhifadhi
  Nimemuona Mungu amefiwa ana majonzi
  Anatamani mimi niende kumfariji
  Nimemuona Mungu ni kilema na hajiwezi
  Anatamani mimi niende kumuinua
 4. Nimemuona Mungu atolewa angali mimba
  Anatamani mimi niende kumtetea
  Nimemuona Mungu anapigwa kwa makombora
  Anatamani mimi niende kusuluhisha
  Nimemuona Mungu ni mtumwa ananyanyaswa
  Anatamani mimi niende kumtetea
Mungu Yulee
ALT TITLENimemuona Mungu
COMPOSERBernard Mukasa
CHOIRSt. Kizito Makuburi
ALBUMMungu Yule
CATEGORYTafakari
 • Comments