Nimeonja Pendo Lako
Nimeonja Pendo Lako | |
---|---|
Alt Title | Nitawainua Wote |
Performed by | Kwaya Kuu ya St. Cecilia Arusha |
Album | Nikiziangalia Mbingu (vol 18) |
Category | Thanksgiving / Shukrani |
Composer | Bernard Mukasa |
Views | 40,838 |
Nimeonja Pendo Lako Lyrics
- Nimeonja pendo lako, nimejua u mwema
Nitakushukuru nitawainua wote wakusifu wewe
Nitawaongoza vyema waimbe kwa furaha
Nitakushukuru nitawainua wote wakusifu wewe.Ukarimu wako Bwana, na huruma yako wewe
Msamaha wako Bwana, na upole wako (wewe)
Umenitendea wema usiopimika
Nitakushukuru nitawainua wote wakusifu wewe - Kina mama simameni, piga vigelegele
Na kina baba nyanyuka mkapige makofi - Watu wote nesanesa chezeni kwa furaha
Inua mikono juu, mshangilieni Bwana - Watawa washangilie, makasisi waimbe
Walei warukeruke, waseme aleluya - Vitambaa mikononi, vipeperushwe juu
Na vichwa viyumbeyumbe kwa mwendo wa kuringa - - Nitakushukuru mimi, na nyumba yangu yote -
Nitayatangaza haya, maisha yangu yote -