{ Nimevipiga vita, nimevipiga vita vilivyo vizuri } *2
{ Mwendo - mwendo nimeumaliza
Mwendo - imani nimeilinda
Mwendo nimeumaliza, imani nimeilinda } *2
- Baada ya hayo nimewekewa taji,
Nimewekewa taji, taji ya ahadi
- Sasa namiminwa, nao wakati wangu
Wa kufariki kwangu, nao umefika
- Ataniokoa na kila neno baya
Hadi niufikie ufalme wa mbingu
- Nami nitaishi kwake Baba milele
Tena nikimwimbia Mungu aleluya
|
|
|