Nimevunja Mkataba
Nimevunja Mkataba | |
---|---|
Performed by | Kwaya Kuu ya St. Cecilia Arusha |
Album | MSHIPI (VOL. 22) |
Category | Tafakari |
Composer | Victor Aloyce Murishiwa |
Views | 12,721 |
Nimevunja Mkataba Lyrics
- Lo Kumbe ni wewe shetani umeniletea matatizo yote haya
Ondoka kwangu haraka kwa jina la Yesu ondoka kwangu
Lo kumbe ni wewe shetani ulisababisha nikamsahau Mungu
Ondoka kwangu haraka kwa jina la Yesu ondoka kwangu{ Nimevunja mkataba na wewe (shetani)
Ondoka, ondoka nasema
Namkaribisha Yesu moyoni mwangu }*2 - Lo kumbe ni wewe shetani ulisababisha nikafungwa gerezani-
Lo kumbe ni wewe shetani nikaipokea rushwa- - Lo kumbe ni wewe shetani ulinipeleka katika nguvu za giza-
Lo kumbe ni wewe shetani uliniongoza katika njia ya dhambi- - Lo kumbe ni wewe shetani unakosanisha ndugu nao majirani-
Lo kumbe ni wewe shetani unasababisha vifo vinakuwa vingi