Nimtume Nani
Nimtume Nani Lyrics
Nimtume nani, unitume mimi, nitume Bwana *2
Nitakwenda kutangaza Neno lako Bwana
Mataifa ya dunia yakufuate wewe
Unitume mimi nitume Bwana
- Bwana asema, nimtume nani
Aende kuwahubiria mataifa?
- Bwana amenituma kuihubiri, habari njema kwa watu
Roho wa Bwana yu juu yangu
- Kwa maana amenitia mafuta
Kuwahubiria maskini habari njema
- Bwana ndiye kiongozi wangu
Anisaidie kuchunga neno lake
// alternative Stanzas //
- Ukingali tumboni mwa mama yako nalikutakasa,
Nalikuita ili uwe mtume wangu.
- Utakwenda kutangaza neno langu,
Usiogope kwa ajili ya hao.
- Mimi katika mashaka na shida zako zote,
Mimi nitakufundisha utakayosema