Ninafikiria Sana
Ninafikiria Sana | |
---|---|
Performed by | St. Paul Students' Choir (University of Nairobi) |
Album | Mbinguni Kutakuwa Raha (Vol 4) |
Category | Tafakari |
Composer | J. C. Shomaly |
Views | 5,801 |
Ninafikiria Sana Lyrics
- Ninafikiria sana na kutafakari jambo hili mimi
Jinsi ulimwengu ulivyogeukageuka kama kinyonga
Ukweli umegeuka na kufanyika kuwa uwongo leo
Msema kweli muovu muongo, yeye wakili wa mambo yote
Shetani mbaya amezizunguka roho za watu
Anawadanganya kwa mambo mazuri pia na anasa,
Kanuni zake ngumu amri zake
nazo zinashangaza shangaza
Mbuzi wa kijani, ng`ombe wa dhambarau
Kuku mwenye pembe, huyo utampata wapi
Njoo kwake Yesu (Mwokozi) hahitaji haya (yote)
Kanuni tubu dhambi, uingie mbinguni kwa baba - Anakudanganya atakupa fedha uwe ni tajiri
Kanuni zake yeye hudhulumu maskini na wajane
Amelaaniwa amelaaniwa afanyaye haya,
Kizazi chake yeye kitakuwa ni laana na fedheha
Maisha yake yeye ni nchi kame na yenye chumvi nyingi - Anakudanganya pombe inaweza kukuliwaza
Utafune mifupa ungali bado ukiwa na meno
Unafanya haya na watoto wako wanalala njaa,
Na wewe kijana wazazi nyumba inawangukia
Mwisho unapotea maisha yako wewe unachemsha - Sikieni sasa enyi mnaoufanya ukahaba
Mkijidanganya miili ni yenu sio ya yeyote
Nani anaweza kujiongeza hata unywele wake
Aliyekulea angefanya hivyo ungekuwa wapi
Na Mungu naye asingekuumba wewe ungekuwa wapi - Sikieni enyi mfanyao vita pia migogoro
Hamuoni kuwa hayo ni machukizo kwake Mwenyezi,
Mungu ameumba nchi nzuri yenye rutuba na mwanga
Na sisi binadamu twaharibu kwa mabomu na risasi
Tukumbuke ya kwamba mwisho tutalipa tutalipa haya - Jukumu ni letu sasa tuzitubu dhambi zetu zote
Tuliyoyafanya tumuombe Mola wetu asamehe,
Tutakuwa safi dunia yote itajaa amani,
Maisha yatakuwa ni rahisi utovu hamna tena,
Na wote tutakuwa jamii yenye maendeleo bora