Ninaikumbuka Siku
   
            Ninaikumbuka Siku Lyrics
 
- Ninaikumbuka siku ile niliyokuita Bwana wangu
 Ukaniponya na kuniepusha na hatari mbaya ya kifo
 Mwili wangu uliopatwa na majeraha makubwa
 Yenye maumivu makali na ya kutisha
 Na ya kukatisha tamaa
 
 {
 /b/
 Nitamke maneno gani, niimbe wimbo gani mimi
 Nicheze ala gani au niipige ngoma gani
 Kama asante na shukrani yangu Bwana
 Na nitoe sadaka gani, iwe kama shukrani yangu
 Nikikumbuka wema wako, nisifuje Bwana wangu
 Wewe ni mwenye huruma na upendo
 
 /w/
 Maneno gani mimi nitamke, na wimbo gani niimbe
 Mimi nipige ngoma gani
 kama asante na shukrani yangu Bwana
 Sadaka nikutolee ee Bwana,
 ni kama shukrani yangu, nikusifuje Bwana wangu,
 Wewe ni mwenye huruma na upendo } * 2
- Ninakumbuka siku ile mimi niliposhindwa
 Na maumivu ya majeraha ya kichwa niliyoyapata
 Maumivu makali mimi yalinibana sana
 Hata mwili ulikosa nguvu na fahamu kunipotea
 (Mimi ) mimi Bwana (niseme) niseme asante
 Kukushukuru ee Mungu wangu
 (Mimi) mimi Bwana (nisipo) nisipotamka nitakuwa sina fadhila
- Ninakumbuka siku ile mikono yangu mimi
 Ilipopatwa na maumivu yaliyotokana na ajali
 Mikono yangu mimi ilitokwa na damu nyingi
 Hata na mifupa yangu iliyovunjika na kutokeza
 (Mimi ) mimi Bwana (niseme) niseme asante
 Kukushukuru ee Mungu wangu
 (Mimi) mimi Bwana (nisipo) nisipotamka nitakuwa sina fadhila
- Nilipopata fahamu nikajaribu kusimama
 Mwili ulikosa nguvu kwa maumivu tena makali
 Miguu yangu inatokwa damu nyingi na kunitisha
 Hata na mifupa yangu iliyovunjika na kutokeza. . .
 (Mimi ) mimi Bwana (niseme) niseme asante
 Kukushukuru ee Mungu wangu
 (Mimi) mimi Bwana (nisipo) nisipotamka nitakuwa sina fadhila
- Usingizi mzito ulinibeba na kunifanya
 Niyasahau maumivu yangu yote niliyo nayo
 Maumivu makali tena ya ndani yalinibana
 Hata kuhema siwezi kugeuka hadi nisaidiwe . . .
 (Mimi ) mimi Bwana (niseme) niseme asante
 Kukushukuru ee Mungu wangu
 (Mimi) mimi Bwana (nisipo) nisipotamka nitakuwa sina fadhila
- Hebu jiulize ndugu ni wangapi wanaopata haya
 Hata uhai wao hutoweka na usirudi
 Jitafakari ndugu wewe uzima uliojaliwa
 Hata asante kwake Muumba tazama umemsahau, .
 (Mimi ) mimi Bwana (niseme) niseme asante
 Kukushukuru ee Mungu wangu
 (Mimi) mimi Bwana (nisipo) nisipotamka nitakuwa sina fadhila