Ninakupenda Mungu
Ninakupenda Mungu | |
---|---|
Alt Title | Pokea Sifa Zangu |
Performed by | Kwaya Kuu ya St. Cecilia Arusha |
Album | MSHIPI (VOL. 22) |
Category | Thanksgiving / Shukrani |
Composer | Victor Aloyce Murishiwa |
Views | 42,082 |
Ninakupenda Mungu Lyrics
Ninakupenda Mungu (wangu)
Ninakupenda wewe milele na milele
(Bwana) nitakutukuza
Pokea sifa zangu (Bwana)
Zinazotoka katika kinywa changu mimi
(ndani) na moyoni mwangu *2- Katika makusanyiko nitaziimba zaburi
Nitazitangaza sifa zako daima milele
Kwenye madhabahu yako nitaitoa sadaka
Ile ya kukupendeza ee Mungu Muumba wangu. - Umenitendea mengi, mema yasiyo idadi
Ninakushukuru Bwana, ee Baba Muumba wangu
Nikiyakumbuka yote, machozi yanimwagika
Ni machozi ya furaha, ni machozi ya upendo. - Usiniache ee Bwana, na wala usinitupe
Ukinitupa wewe, nani ataniokota
Ndiwe msitiri wangu, katika dunia hii
Dunia yenye mateso na yenye mahangaiko