Login | Register

Sauti za Kuimba

Ninakupenda Mungu Lyrics

NINAKUPENDA MUNGU

@ Victor Aloyce Murishiwa

Ninakupenda Mungu (wangu)
Ninakupenda wewe milele na milele
(Bwana) nitakutukuza
Pokea sifa zangu (Bwana)
Zinazotoka katika kinywa changu mimi
(ndani) na moyoni mwangu *2

 1. Katika makusanyiko nitaziimba zaburi
  Nitazitangaza sifa zako daima milele
  Kwenye madhabahu yako nitaitoa sadaka
  Ile ya kukupendeza ee Mungu Muumba wangu.
 2. Umenitendea mengi, mema yasiyo idadi
  Ninakushukuru Bwana, ee Baba Muumba wangu
  Nikiyakumbuka yote, machozi yanimwagika
  Ni machozi ya furaha, ni machozi ya upendo.
 3. Usiniache ee Bwana, na wala usinitupe
  Ukinitupa wewe, nani ataniokota
  Ndiwe msitiri wangu, katika dunia hii
  Dunia yenye mateso na yenye mahangaiko
Ninakupenda Mungu
ALT TITLEPokea Sifa Zangu
COMPOSERVictor Aloyce Murishiwa
CHOIRKwaya Kuu ya St. Cecilia Arusha
ALBUMMSHIPI (VOL. 22)
CATEGORYThanksgiving / Shukrani
MUSIC KEYE Major
TIME SIGNATURE6
16
SOURCESt. Theresa Cathedral Arusha Tanzania
NOTES Open PDF
 • Comments