Login | Register

Sauti za Kuimba

Ninazo sababu Lyrics

NINAZO SABABU

@ Alfred Ossonga

Ninazo sababu za kutoa shukrani zangu
Ninakushukuru Bwana kwa ukarimu wako
Ee Baba asante [sana] kwa upendo wako
Pokea zawadi [hii], ninakutolea
 

 1. Enyi watu wa Mungu, njooni kwa masifu
  Kusanyikeni leo, mbele zake Bwana
  [Piga] pi- kelele, [piga] piga ngoma
  [Shangwe] sha- deremo, [piga] piga ‘kofi
  Â
 2. Mbingu pia dunia, ni mali ya Bwana
  Mito pia bahari, ni mali ya Bwana
  [Tuna]tu- sababu, [za ku]za- shukuru
  [Bwana]bwa- pokea, [shukra]shu- ni zetu
  Â
 3. Uhai wangu mimi, ni mali ya Bwana
  Sauti yangu nzuri, Bwana amenipa
  [Bwana] bwa- asante, [kwa we] kwa- ‘ma  wako
  [Naku] na- kwimbia, [naku] kuinua
  Â
 4. Natembea mchana, Bwana aniongoza
  Ninalala usiku, Bwana hunilinda
  [Bwana] bwa- asante, [kwa we] kwa- ‘ma  wako
  [Naku] na- shukuru, [naku] kutukuza
Ninazo sababu
COMPOSERAlfred Ossonga
CHOIRSt. Francis of Assisi Kariobangi
ALBUMPaazeni Sauti
CATEGORYThanksgiving / Shukrani
 • Comments