Ningekuwa na Mabawa
Ningekuwa na Mabawa Lyrics
Ningekuwa na mabawa, ningeruka hadi mbinguni
Ningekuwa na ufunguo, ningefungua mlango wako
{ Niingie nyumbani mwako, nikuimbie Mungu wangu
Katika makao yako, makao ya milele } *2
- Malaika wanakuimbia nyimbo nzuri za furaha.
Makerubi hata maserafi wanasifu jina lako
- Ningekuwa mimi ni bahari ningevuma kwa sauti
Ningekuwa mimi ni kengele ningelia usikie
- Bwana mimi nitakuimbia siku za maisha yangu
Nitaimba sifa zako Bwana ili watu wasikie
- Naamini kwamba siku moja nitafika mbele zako
Natamani sana kuja kwako kwenye raha ya milele