Login | Register

Sauti za Kuimba

Ningekuwa na Mabawa Lyrics

NINGEKUWA NA MABAWA

@ Alfred Ossonga

Ningekuwa na mabawa, ningeruka hadi mbinguni
Ningekuwa na ufunguo, ningefungua mlango wako
{ Niingie nyumbani mwako, nikuimbie Mungu wangu
Katika makao yako, makao ya milele } *2

 1. Malaika wanakuimbia nyimbo nzuri za furaha.
  Makerubi hata maserafi wanasifu jina lako
 2. Ningekuwa mimi ni bahari ningevuma kwa sauti
  Ningekuwa mimi ni kengele ningelia usikie
 3. Bwana mimi nitakuimbia siku za maisha yangu
  Nitaimba sifa zako Bwana ili watu wasikie
 4. Naamini kwamba siku moja nitafika mbele zako
  Natamani sana kuja kwako kwenye raha ya milele
Ningekuwa na Mabawa
COMPOSERAlfred Ossonga
CHOIRSt. Joseph Migori
ALBUMMabawa
CATEGORYEntrance / Mwanzo
 • Comments