Ningelikuwa Kengele
Ningelikuwa Kengele | |
---|---|
Performed by | St. Paul Students' Choir (University of Nairobi) |
Album | Habari Tuliyoleta (Vol 6) |
Category | Thanksgiving / Shukrani |
Composer | J. C. Shomaly |
Views | 4,350 |
Ningelikuwa Kengele Lyrics
Ningelikuwa ni kengele mimi ningelia usikie!
Ningelikuwa ni maua mimi ningechanua chanua
Ili niupambe uso wako ewe Mungu uliyeniumba
(Tena mimi) ukanipatia akili na mali ili nikutumikie
{ Naona fahari ninapotamka maneno haya,
Ninapotazama kwa jinsi ulivyonipenda mimi kupita upeo } *2- Umetamalaki Mungu (Mungu wangu),
Nikulipe nini Bwana (hakika)
Kila ninapotazama, wanadamu tulivyoumbika - Akili na maarifa (yote hayo)
Umetupatia Mungu (tazama)
Sisi viumbe pekee, utashi nao ukatujaza - Neema zako ni kuu (sana sana)
Kwa wanao wote Baba (hakika),
Mvua yako wainyesha hata kwa viumbe wenye dhambi - Shukurani ninatoa (mimi Bwana),
Kiumbe mnyonge Baba (naomba),
Wabariki mayatima, na wale wasio na uwezo