Login | Register

Sauti za Kuimba

Ningelikuwa Kengele Lyrics

NINGELIKUWA KENGELE

@ J. C. Shomaly

Ningelikuwa ni kengele mimi ningelia usikie!
Ningelikuwa ni maua mimi ningechanua chanua
Ili niupambe uso wako ewe Mungu uliyeniumba
(Tena mimi) ukanipatia akili na mali ili nikutumikie
{ Naona fahari ninapotamka maneno haya,
Ninapotazama kwa jinsi ulivyonipenda mimi kupita upeo } *2

 1. Umetamalaki Mungu (Mungu wangu),
  Nikulipe nini Bwana (hakika)
  Kila ninapotazama, wanadamu tulivyoumbika
 2. Akili na maarifa (yote hayo)
  Umetupatia Mungu (tazama)
  Sisi viumbe pekee, utashi nao ukatujaza
 3. Neema zako ni kuu (sana sana)
  Kwa wanao wote Baba (hakika),
  Mvua yako wainyesha hata kwa viumbe wenye dhambi
 4. Shukurani ninatoa (mimi Bwana),
  Kiumbe mnyonge Baba (naomba),
  Wabariki mayatima, na wale wasio na uwezo
Ningelikuwa Kengele
COMPOSERJ. C. Shomaly
CHOIRSt. Paul Students' Choir (University of Nairobi)
ALBUMHabari Tuliyoleta (Vol 6)
CATEGORYThanksgiving / Shukrani
 • Comments