Niseme Nini Basi
Niseme Nini Basi Lyrics
{ Niseme nini basi juu ya mama Yetu Maria
(Mama Bikira Maria)
Mama mpendelevu mama mwenye neema } *2
- Wakati wa majaribu, mwombezi wetu ni Maria (Mama yetu)
Wakati wa mashaka kimbilio letu ni Mama (Maria)
- Mama uliyeumbwa, pasipo dhambi ya asili
Ukamzaa mwanao mkombozi wa walimwengu
- Moyo wako wa heri moyo safi moyo mweupe
Nijalie neema nishinde majaribu yote
- Mama wa Mkombozi mnara wetu wa Mbinguni
Mwangaza wetu sisi tunaosafiri gizani
- Shika mkono wangu unionyeshe njia ya kweli
Nifike kwa Mwanao anakoketi uwinguni